pmbet

Musiisahau ukraine wakati wa vita dhidi ya iran - Zelensky

Eric Buyanza

March 21, 2026
Share :

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amewatolea wito washirika wa Magharibi kutoisahau nchi yake wakati huu macho yakielekezwa Mashariki ya Kati kufuatia vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.
 

Akizungumza akiwa ziarani nchini Uingereza, Zelensky alijaribu kuonesha mfanano baina ya tawala za Urusi na Iran, ambazo kwa maneno yake ni "ndugu wanaounganishwa na chuki zao", na kwamba tawala za aina hiyo “kamwe haziwezi kuachiwa zikashinda.”
 

Hata hivyo, rais huyo wa  Ukraine ambaye alikuwa jijini London kusaka uungaji mkono zaidi wa Waziri Mkuu Keir Starmer, alisema mbele ya mwenyeji wake huyo kwamba bado juhudi za kidiplomasia ni muhimu kumaliza vita nchini mwake.
 

"Pia, bila kusahau kuhusiana na juhudi zetu za kidiplomasia na mazungumzo na pale tulipo na Wamarekani na Warusi, tunapaswa kujadili mada hii tete. Na bila shaka kuhusu Mashariki ya Kati. Hili lina athari kubwa kwetu Ukraine na kwa Ulaya nzima." Alisema Zelensky.
 

Akiunga mkono maneno ya mgeni wake,  Starmeralisema licha ya vita kwenye Mashariki ya Kati kubeba uzito mkubwa kutokana na kuhusisha kwake pande nyingi kwa wakati mmoja, dunia inapaswa kuendelea kulishughulikia suala la vita vya Urusi nchini Ukraine na kulimaliza haraka iwezekanavyo.
 

"Hapana shaka kuna mgogoro wa Iran unaoendelea kwenye eneo la Mashariki ya Kati, lakini hatuwezi kupoteza umakini wetu kwa kile kinachoendelea nchini Ukraine na haja ya kuunga mkono huko. Na pili, ni muhimu sana kuwa wawazi kwamba Putin hawezi kuwa mfaidikaji wa mgogoro wa Iran, ama iwe ni kwenye bei za mafuta ama kuondoshwa kwa vikwazo." Alisema Starmer.


 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet