pmbet

Muuaji wa Argentina fainali ya kombe la dunia asajiliwa na PSG

Eric Buyanza

August 15, 2026
Share :

Ferran Torres, ambaye aliifungia Hispania bao la ushindi kwenye Kombe la Dunia, amejiunga na Paris Saint-Germain (PSG), mabingwa wa Ulaya, akitokea Barcelona.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amesaini mkataba na mabingwa hao wa Ufaransa hadi mwaka 2031, kwa ada inayoripotiwa kufikia takribani pauni £42.7 milioni, ambazo ni sawa na TSh bilioni 153.1.

 

Mwezi uliopita, Torres alifunga bao la ushindi katika muda wa nyongeza dhidi ya Argentina, na kuisaidia Hispania kutwaa Kombe lao la pili la Dunia kwa upande wa wanaume.
 

Ferran Torres alifunga mabao 21 katika michezo 49 katika mashindano yote, huku akitoa assist 3, huku akiisaidia Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huo.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet