Muunganiko Simba unahitaji muda, mashabiki wapewa angalizo
Eric Buyanza
July 26, 2024
Share :
Nyota wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ amekisifia kikosi kipya cha Simba, lakini akatoa angalizo kwa kusema ni ngumu kwa timu yenye idadi kubwa ya wachezaji wapya kufanya vizuri ndani ya kipindi kifupi, hivyo ni vyema mashabiki wa Msimbazi kutambua hilo wakati kocha wao, Fadlu Davids akiendelea kukisuka upya.
“Ninachokiona kwa sasa kocha anapambana kupata muunganiko, hili ni jambo ambalo huwa linahitaji muda, kama ikitokea wakielewana kwa haraka hiyo itakuwa bahati, natamani mashabiki wa Simba waonyeshe ukomavu kwa kuwa nyuma ya timu yao hasa kipindi hiki ambacho inajengwa,” alisema Mogella.
MWANASPOTI