Mvua kuendelea kupiga mikoa ya kanda ya ziwa
Sisti Herman
March 4, 2026
Share :

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa angalizo la mvua kubwa kuanzia jana Jumatano, Machi 4, 2026 katika maeneo machache ya mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Kigoma, Katavi na Tabora.
Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Jumanne, Machi 3, 2026 imeeleza athari zinazoweza kujitokeza kwa baadhi ya maeneo ya makazi ni kuzungukwa na maji, hivyo imewataka wananchi kuzingatia hilo na kujiandaa.
Aidha, mvua hizo zitaendelea Alhamisi Machi 5, 2026 katika maeneo ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Mara, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.





