Mvua yabomoa nyumba na madarasa
Eric Buyanza
April 9, 2024
Share :
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo, imebomoa nyumba 17 huku nyingine 61 zikiezuliwa mapaa katika Kijiji cha Lyasembe, Kata ya Murangi, jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara.
Tukio hilo lilitokea Machi 5 mwaka huu, huku watu 685 wakiathirika wakiwamo watoto 384 na watu wazima 301, lakini pia vyumba viwili vya madarasa ya Shule ya Msingi Lyaembe vikibomoka.