Mvua yakwamisha mechi ya TRA na Simba kupigwa Arusha.
Joyce Shedrack
March 14, 2026
Share :
Mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya TRA United vs Simba SC iliyopangwa kuchezwa leo saa 10:00 jioni, imeahirishwa kutokana hali ya uwanja iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha jijini Arusha.
Kamishna wa mchezo huo Mussa Nyamandege amethibitisha kuahirisha mchezo huo akisema ametumia sheria namba moja ya mchezo wa mpira wa miguu kufanya hivyo akidai kuwa mpira hauwezi kudunda baada ya uwanja kujaa maji.
Taarifa zaidi kuhusu hatma ya mechi hii itatolewa baadaye na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).





