Mvua zasababisha bwawa kupasua kingo, 42 wapoteza maisha
Eric Buyanza
April 29, 2024
Share :
Watu 42 wamepoteza maisha baada bwawa la Kijabe kuvunja kingo zake katika eneo la Mahi-Mahiu nchini Kenya.
Inaelezwa kuwa bwawa hilo lilivunja kingo zake alfajiri ya kuamkia leo (Jumatatu) baada ya kuzidiwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Maji yalisambaa kwenye mitaa iliyo karibu na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa wa barabara kuu ya Nairobi-Nakuru huku yakisomba nyumba na magari.
Moja ya magari yaliyosombwa na maji hayo ni basi la kampuni ya Easy Coach lililokuwa na watu 60.