Mvua zinazoendelea kunyesha zabomoa ukuta wa gereza, wafungwa 119 wahofiwa kutoroka
Eric Buyanza
April 26, 2024
Share :
Mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa kadhaa katika mji wa Suleja nchini Nigeria, imeharibu majengo na uzio wa gereza kusababisha kutoroka kwa jumla ya wafungwa 119 amesema msemaji wa mamlaka ya magereza ya Nigeria, Adamu Duza.
Mamlaka ya magereza imetoa wito kwa wananchi kuwa makini na wafungwa waliotoroka na kutoa taarifa kwa maafisa wa usalama.
Kutoroka ni jambo la kawaida katika magereza yenye msongamano mkubwa nchini Nigeria, itakumbukwa mwezi Julai 2022, wana-Jihadi waliingia kwenye gereza la Kuje nje kidogo ya mji wa Abuja wakiwa na vilipuzi na silaha nzito, na kuwaachilia wafungwa zaidi ya 800, wakiwemo wenzao zaidi ya 60.