pmbet

Mwaka 2020 alikamatwa na polisi kesho ni hakimu fainali ya Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

July 18, 2026
Share :

Mwamuzi wa kimataifa kutoka Slovenia, Slavko Vinčić, ameandika ukurasa mpya katika maisha yake ya uamuzi baada ya FIFA kumteua kuchezesha fainali ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Hispania na Argentina.

FIFA Appoints Slavko Vinčić as Referee for 2026 World Cup Final Between  Spain and Argentina

Uteuzi huo unakuja miaka sita baada ya Vinčić kukamatwa na polisi nchini Bosnia mwaka 2020 wakati wa operesheni iliyolenga kuvunja mtandao wa uhalifu. 

 

Hata hivyo, mwamuzi huyo aliachiliwa baadaye bila kufunguliwa mashtaka yoyote, huku Shirikisho la Soka la Slovenia likimtetea hadharani na kusisitiza kuwa hakuhusika na kosa lolote.

 

Licha ya tukio hilo kuzua mjadala mkubwa wakati huo, Vinčić aliendelea na kazi yake ya uamuzi na sasa amepewa heshima kubwa zaidi katika taaluma yake kwa kuteuliwa kusimamia mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia.

 

Katika mechi hiyo ya kihistoria, Vinčić atasaidiwa na waamuzi wenzake kutoka Slovenia, Tomaž Klančnik na Andraž Kovačič, huku Adham Makhadmeh akiwa mwamuzi wa nne na Mohammad Alkalaf akiteuliwa kuwa mwamuzi msaidizi wa akiba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet