Mwaka 2023, watu 163,131 waligundulika na maambukizi ya ukimwi - Ummy
Eric Buyanza
January 13, 2024
Share :
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema watu 163,131 waligundulika kuwa na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa mwaka 2023.
Ummy aliyasema hayo wiki hii jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini kwa mwaka 2023.
Kwa mujibu wa taarifa hizo jumla ya watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) mwaka jana na watu 163,131 walingundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo....ukilinganisha na watu 182,095 waliogundulika mwaka jana.
Aidha, amesema waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU walikuwa 1,663,651.
“Mwaka 2023, vifo vitokanavyo na UKIMWI vilikuwa 22,000 kulinganisha na vifo 29,000 mwaka 2022(Spectrum 2022),”amesema Ummy.