pmbet

Mwaka 2024 kulikuwa na ongezeko la mabilionea wapya 204

Eric Buyanza

January 20, 2025
Share :

Shirika la kimataifa la kutoa misaada la Oxfam limesema utajiri wa mabilionea duniani, uliongezeka mara tatu zaidi mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2023.

Ripoti mpya ya shirika hilo iliyotolewa kabla ya jukwaa la kimataifa la kiuchumi linalotarajiwa kufanyika huko Davos, inaonya kuhusu nguvu kubwa ya kisiasa na kiuchumi inachipuka kutoka kwa matajiri hao na kuutaja kuwa mfumo wa matajiri wachache walio na ushawishi mkubwa.

Oxfam inabashiri kuwa matajiri watanufaika pakubwa na kurejea uongozini kwa Rais wa Marekani Donald Trump na kusababisha kuongezeka kwa pengo la ukosefu wa usawa kati ya matajiri na masikini katika jamii.

Wametoa mfano wa mmiliki wa kampuni ya magari ya kifahari ya Tesla ambaye pia anamiliki mtandao wa kijamii wa X Elon Musk ambaye alifadhili pakubwa kampeini za Trump.

Matajiri watatu wakubwa ulinwenguni Leon Musk,Jeff Bezos wa kampuni ya Amazon na Mark Zuckerberg wa kampuni ya Meta watakuwa katika hafla ya kuapishwa kwa Donald Trump.

Mkurugenzi mkuu wa Oxfam Amitabh Behar amesema wanatoa ripoti huyo kuangazia namna watu wa kawaida kote ulimwenguni wanateseka huku wachache wakiwa na mali nyingi kupita kiasi.

Utajiri wa mabilionea hao uliongezeka kwa dola trilioni mbili zaidi mwaka jana na kufikia utajiri jumla wa dola trilioni kumi na tano.Ripoti hiyo imebaini mwaka jana kulikuwa na mabilionea 204 wapya na kufikisha idadi ya mabilionea ulimwenguni kufika 2,769.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet