Mwaka wa maajabu kwa Kobbie Mainoo
Sisti Herman
March 24, 2024
Share :
Ikiwa ni miezi minne tu tangu acheze mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya wakubwa ya Manchester United na kuwaka vilivyo kinda Mwingereza Kobbie Mainoo jana amecheza mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya Taifa akiwa na miaka 18 tu.
Kwenye mchezo huo waliopoteza 1-0 dhidi ya Brazil, Mainoo aliingia akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya kiungo wa klabu ya Chelsea Conor Callagher na kwenda kucheza kiungo wa kati sambamba na Declan Rice.