pmbet

Mwakinyo arejea namba 1 Afrika

Sisti Herman

January 6, 2026
Share :

 

Bondia maarufu zaidi Tanzania Hassan Mwakinyo amerejea rasmi kwenye orodha ya viwango ya mabondia wanaotambulika na mtandao wa ngumi Duniani, Boxrec huku akiwa nafasi ya kwanza kwa uzito wa kati 'Middle' barani Afrika.

Mwakinyo amerejea juu kwenye orodha za Boxrec baada ya Desemba 26, 2025 Mwakinyo kucheza pambano la kimataifa dhidi ya bondia Mnigeria, Stanley Eribo na kushinda kwa ‘KO’ raundi ya pili.

Kwa upande wa orodha ya jumla ya mabondia bora nchini Tanzania, Mwakinyo ameshika nafasi ya pili nyuma ya bondia chipukizi Salmini Kassim huku mpinzani wake Twaha Kiduku akishika nafasi ya 27 akiwa na nyota mbili.

Mwaka 2025 Mwakinyo alicheza pambano moja pekee ambalo limemrudisha kwenye ubora huo lakini hasimu wake Twaha Kiduku amecheza mapambano mawili na kushikilia nafasi ya 27 na kwa upande wa Mfaume Mafume aliyecheza pambano moja mwaka wa jana ameshika nafasi ya 127 akiwa na nyota moja katika orodha ya jumla ya mabondia wote bora wa Tanzania ambao bado wapo kwenye ‘game’

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet