Mwakinyo kupeperusha bendera ya Tanzania June 10 Ivory Coast
Sisti Herman
June 9, 2026
Share :

Bondia wa Kitanzania, Hassan Mwakinyo anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania Juni 10, 2026 Nchini Ivory Coast katika pambano la kuwania ubingwa wa IBO Africa Middle Weight dhidi ya Michel Soro.
Mashabiki wa Mwakinyo ‘Champez’ wanatarajia kiwango bora chenye hadhi ya Kimataifa na kuipeperusha vyema bendera ya Taifa katika mashindano hayo.
Aidha mbali na Mwakinyo, Mabondia wengine wa Tanzania watakaopanda ulingoni katika usiku huo wa ngumi ni Richard Mtangi pamoja na Amiri Rashidi Matumla, ambaye ni mtoto wa nguli wa ngumi nchini, Rashidi Matumla.





