Mwakinyo kurejea ulingoni disemba 26 mwaka huu.
Joyce Shedrack
August 15, 2025
Share :
Bondia wa Ngumi za Kulipwa nchini Hassan Mwakinyo ametangaza kurejea ulingoni katika pambano la kimataifa la Ubingwa Wa Afrika Jijini Mwanza Desemba 26 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari siku ya leo Jijini Dar es Salaam Mwakinyo, amesema anawaomba wadhamini wajitokeze kwa pambano hilo la "BOX ON BOXING DAY" ili kukata kiu ya mashabiki ngumi.
Pambano la "Boxing on Boxing Day" linatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza Jijini Mwanza ambapo Hassan Mwakinyo atapanda ulingoni kwa ajili ya kukata kiu ya mashabiki wa masunbwi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.





