MWAKINYO: "Niko tayari asilimia zote kuzichapa na mkongo"
Eric Buyanza
January 23, 2024
Share :
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya pambano lake dhidi ya Mbiya Kanku litakalofanyika Januari 27, 2024 kwenye uwanja wa Amani Complex Indoor Arena, Zanzibar....bondia Hassan Mwakinyo amesema yuko kamili kwenye kila idara kwa asilimia 98.|
Mwakinyo ambaye atapambana na Kanku raia wa DR Congo wanatarajiwa kupanda ulingoni katika pambano la ubingwa wa WBO Afrika, anasema mikono yake iko tayari kuongea ulingoni na amewatoa hofu mashabiki wa masumbwi visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuwa siku hiyo ataonesha burudani ya kuvutia.
Mapambano mengine yatakayopigwa siku hiyo; Hussein Itaba dhidi ya Juma Misumari wa Morogoro, Bakari H.Bakari na Seleman Hamad, Masoud Khatibu atazichapa na Yahaya Khamis, huku mwanadada Zulfa Iddi akivaana na Debora Mwenda.