Mwalimu ajikuta kwenye orodha ya wapiga kelele darasani
Eric Buyanza
February 4, 2025
Share :
Mwalimu mmoja wa shule ya msingi huko nchini Nigeria 'ameshea' kupitia mtandao wake wa TikTok orodha iliyowasilishwa kwake na mwanafunzi aliyempa jukumu la kuandika majina ya wapiga kelele darasani.
Mwalimu huyo aliyefahamika kwa jina Chinwe, anasema alishtuka baada ya kukuta jina lake kwenye karatasi hiyo na alipomuuliza mwanafunzi huyo ni kwanini? Akajibiwa na wewe ulikuwa ukipiga kelele.