pmbet

Mwalimu akamatwa kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi ofisini kwake.

Joyce Shedrack

March 20, 2025
Share :

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mwalimu wa Shule ya Sekondari Zombo iliyopo Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili (16).

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro ametaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Makame Mwaisumo (30), ambapo anadaiwa kufanya kosa hilo majira ya asubuhi, Machi 19 mwaka huu, ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu baada ya kumtuma akachukue andalio la somo.

RPC Mkama amesema baada ya mwanafunzi huyo kwenda ofisini alikokuwa ametumwa, mwalimu huyo alimfuata ndani na kumfanyia ukatili huo.

Kwa sasa mwalimu anaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Mwalimu huyo alikuwa akikaimu nafasi ya Mkuu wa Shule na uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo ni mmomonyoko wa kimaadili kwa mwalimu huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet