pmbet

Mwalimu mbaroni kwa kubaka mwanafunzi wa kidato cha 3

Eric Buyanza

May 10, 2024
Share :

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Katoro (jina linahifadhiwa) anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu baada ya kumtuma nyumbani kwake na kisha kumfuata na kumfanyia tendo hilo, tukio lililotokea Mei 2 Mwaka huu.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Safia Jongo, ambaye amesema siku ya tukio, mwanafunzi huyo alikuwa darasani ndipo mwalimu huyo alimwagiza  kwenda nyumbani kwake kumchukulia kitu huku akimfuata kwa nyuma.

Amesema binti huyo alipofika nyumbani kwa mwalimu huyo, alishtuka kuona mlango unafungwa kisha kuanza kufanyiwa ukatili na mwalimu.

SACP Jongo amesema baada ya tukio hilo, mwanafunzi alikwenda kutoa taarifa  kwa mkuu wa shule, na kwamba mkuu huyo kwa kushirikiana na mtuhumiwa walimtisha kuwa watamwadhibu kama atatoa taarifa sehemu yoyote. 

“Tulipata tarifa Mei 5 na kuchukua hatua ya kumkatamata mtuhumiwa pamoja na mkuu wa shule na baada ya hapo, utaratibu wa kisheria unaendelea na hatua zaidi zitachukuliwa dhii yao baada ya kukamilisha uchunguzi,” amesema Kamanda Jongo.

Aidha, kamanda huyo amewataka wazazi, walimu na walezi kuwa na tabia ya kuwahoji watoto wanapotoka shuleni ili kama kuna matatizo wanakumbana nayo, wayabaini mapema. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet