Mwalimu mbaroni kwa kushiriki ngono na denti wa miaka 16
Eric Buyanza
May 14, 2026
Share :

Mwalimu wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 25 kutoka kaunti ya Whitman, Washington nchini Marekani, amekamatwa baada ya kudaiwa kukiri kwa mumewe kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mvulana wa miaka 16.
Mackenzie Naught, ambaye ameolewa kwa miaka minne na kufundisha katika Shule ya Ushirika ya St. John-Endicott tangu 2025, inasemekana alimfahamu kijana huyo kupitia familia yake.
Hati za mahakama zinadai kuwa alikuwa akitaniana naye kwenye Snapchat, na kumshinikiza wakutane katikati ya usiku na kufanya mapenzi kwenye gari.
Mumewe aligundua hilo baada ya kupata ushahidi wa meseji kwenye simu ya mkewe na kuwapa polisi.
Naught anakabiliwa na shtaka la jinai la uhalifu wa kingono na mtoto mdogo.
Kesi hii imeibua hisia kali kwenye jamii kutoakana na uaminifu wanaopewa walimu na wazazi na kuutumia vibaya.





