Mwalimu mdosi asimamishwa kazi kwa kuwaita wanafunzi nyani
Eric Buyanza
February 13, 2024
Share :
Mwalimu wa kidosi (mhindi) aliyefahamika kwa jina la Tayabah Jadwat, anayefundisha shule ya
Curro Academy Protea Glen iliyoko huko Soweto nchini Afrika Kusini, amesimamishwa kazi kufuatia tuhuma za ubaguzi wa rangi.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, alidaiwa kuwaita wanafunzi watatu nyani baada ya wanafunzi hao kuwa wasumbufu darasani jambo ambalo lilifanywa siri na walimu wenzake mpaka lilipokuja kubumburuka hivi karibuni.
Katika taarifa yake Curro Holdings mmiliki wa shule hiyo, alisema alifahamu kuhusu tukio hilo Ijumaa iliyopita na kuanzisha uchunguzi ambapo inaaminika tukio hilo lilitokea katika muhula wa kwanza wa mwaka jana.
"Kutokana na taarifa za tuhuma hizo, Curro amemsimamisha kazi mwalimu mara moja na kuanzisha uchunguzi wa kinidhamu kwa mujibu wa sera na taratibu za kazi.