pmbet

Mwalimu wa hisabati ajiua baada ya kuliwa kwenye kamari

Eric Buyanza

June 8, 2024
Share :

Mwalimu wa sekondari ya Nyamira nchini Kenya aliyefahamika kwa jina la Kelvin Omwenga amejiua baada ya kuliwa pesa nyingi kwenye mchezo wa kamari ya mtandanoni.

Mkuu wa shule ya Nyamira Boys, George Onkundi alisema Omwenga aliajiriwa na shule hiyo miaka 4 iliyopita na alikuwa akifundisha hisabati na kemia.

Alisema Omwenga hakuwahi kuonyesha dalili zozote za msongo 'Stress' lakini akaongeza kuwa mwalimu huyo alikuwa akikopa pesa mara kwa mara kutoka kwa walimu wenzake. 

Mwalimu mwingine ambaye hakupenda jina lake litajwe aliliambia gazeti la Daily Nation kwamba Omwenga alikopa pesa kutoka kwake mara kwa mara, akiahidi kulipa karibuni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet