pmbet

Mwalimu wa madrasa atupwa jela mika 30 kwa kulawiti mwanafunzi wake

Eric Buyanza

March 16, 2024
Share :

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, aliyekuwa mwalimu wa madrasa katika Msikiti wa Ushirika wilayani hapo,  Abdalah Selemani (37), baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 12.
 

Hukumu hiyo ilitolewa  jana na Hakimu Mkazi Nasra Mwashee ambaye alisema  mahakama imeridhika bila kuacha shaka na ushahidi uliotolewa kuhusu kitendo hicho ambacho ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 154(1) (a) cha Kanuni za Adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.
 

Alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwake   na watu wengine wenye tabia ya  kufanya vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto kwenye jamii na kuongeza kuwa ukatili kwa watoto hasa ubakaji na ulawiti, vimekuwa vikitokea mara kwa mara kwenye wilaya ya Nzega na adhabu hizo zitakuwa ni fundisho kwa wengine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet