pmbet

Mwamba huyu hapa, Frank Kessie awaliza Senegal Jiooooni

Sisti Herman

January 30, 2024
Share :

Katika hali ambayo haikutarajiwa na asilimia kubwa ya mashabiki wa soka ulimwenguni, timu ya taifa ya Ivory Coast imevuka mtihani mzito wa kuwatoa mabingwa watetezi wa kombe la mataifa Afrika, timu ya taifa ya Senegal kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 kwenye dakika 90 za mchezo.

 

Frank Kessie ndiye nahodha aliyeokoa jahazi la matokeo kwa wenyeji wa michuano, Ivory Coast dhidi ya mawimbi mazito ya wababe wa Afrika Senegal kwani licha ya kutoanza kwenye majina 11 yaliyoanza aliweza kuisaidia Ivory Coast kusawazisha goli walilotanguliwa na mshambuliaji wa Senegal Habib Diallo huku akitokea benchi.

 

Baada ya hapo nahodha huyo pia alisaidia Ivory Coast kuvuka hatua hiyo kwani ndiye aliyeweza kupiga mkwaju wa penalti wa tano ambao uliwapa ushindi baada ya Senegal kukosa mkwaju mmoja.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet