pmbet

Mwamuzi afungiwa maisha, baada ya kufumwa akishangilia ushindi wa timu aliyoibeba

Eric Buyanza

May 23, 2024
Share :

Huko nchini Uholanzi mwamuzi wa mpira wa miguu 'amesimamishwa kazi maisha' akidaiwa kusherehekea ushindi wa klabu ambayo aliibeba ili ishinde kwa kuwaondoa wachezaji 3 wa klabu pinzani(kwa kadi nyekundu) huku akitoa dakika 15 za nyongeza, zilizotosha kwa ya timu ya St George kupata ushindi muhimu.
 

Mapema mwezi huu, vilabu vya St. George na SV De Valken vilikutana katika mchezo wa mwisho ya ligi ya daraja la nne...mechi iliyokuwa inatakiwa iamue ni timu gani kati ya hizo mbili itapanda daraja.
 

Hata hivyo mchezo ulienda kinyume na ilivyotarajiwa baada ya mwamuzi wa mchezo Bwana Jan Smit kuonyesha mapenzi na upendeleo wa wazi kwa timu ya St George.

Jan Smit anashutumiwa sio tu kwa kupanga matokeo bali pia kwa kusherehekea ushindi wa timu hiyo aliyoibeba.
 

Kwenye mchezo huo, mwamuzi alionyesha kadi 3 nyekundu kwa wachezaji wa SV De Valken na ya 4 kwa kocha wa timu hiyo, na kisha kuongeza dakika 15 za ziada baada ya dakika 90 kutamatika...ambapo pale tu St. George walipofanikiwa kupata bao alipuliza filimbi ya kumaliza mchezo bila kuchelewa.
 

Viongozi wa SV De Valken walilalamika sana baada ya mchezo lakini kilichoibua hasira yao zaidi ni video iliyokuwa ikisambaa mtandaoni ya wachezaji na maafisa wa timu ya St. George wakisherehekea timu yao kupanda daraja wakiwa pamoja na mwamuzi huyo.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet