Mwamuzi aliyeibeba Madrid awaomba radhi Bayern
Sisti Herman
May 9, 2024
Share :
Beki wa klabu ya Bayern Munich Mathias De Ligt baada ya mchezo wao wa hatua ya mtoano dhidi ya Real Madrid kuisha huku wakitolewa kwenye hatua hiyo kwa jumla ya magoli 4-3, nyumbani na ugenini amefunguka kuwa mwamuzi wa pembeni wa mchezo huo alimfuata kumuomba radhi kwa kukataa goli lao.
"Hii ni aibu, mwamuzi wa pembeni amenifuata na kuniambia 'samahani nimefanya makosa' kwa kutafsiri vibaya maamuzi" alisema De Ligt kuhusiana na tukio la goli la Bayern lililokataliwa na waamuzi kwakusema kuwa wachezaji wa Bayern walikuwa wameotea.
Hata hivyo lawama kwa waamuzi hao ziliendelea kwani kwenye mkutano wake na wanahabari kocha Thomas Tuchel alifunguka mengi hasi kuhusiana na maamuzi ya waamuzi hao.
Bayern walipoteza 2-1 Santiago Bernabeu huku wakiwa walitangulia kufunga kwa goli la Alphonso Davies alilofunga dakika ya 68 kabla ya Joselu kusawazisha na kuongeza goli la ushindi dakika 88 na 91.