pmbet

Mwamuzi pekee kutoka CECAFA kuchezesha Kombe la dunia

Sisti Herman

April 13, 2026
Share :

 

Mwamuzi wa soka kutoka Somalia, Omar Artan, ameandika historia baada ya kuteuliwa kuwa Mwamuzi wa kwanza kutoka taifa hilo kuchezesha michuano ya Kombe la Dunia na mwamuzi pekee kutoka ukanda wa CECAFA.

Artan, mwenye umri wa miaka 34, ni miongoni mwa waamuzi 52 walioteuliwa na FIFA kusimamia mechi za fainali zitakazofanyika Canada, Mexico na Marekani.

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, alimpongeza Artan kwa juhudi na weledi wake, akisema mafanikio hayo yameongeza heshima ya Somalia kimataifa.

Artan alianza kuwa mwamuzi wa FIFA mwaka 2018, na tayari amechezesha mashindano makubwa barani Afrika ikiwemo AFCON na Ligi ya Mabingwa Afrika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet