Mwamuzi wa AFCON 2025 Apewa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Joyce Shedrack
May 4, 2026
Share :
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemtangaza mwamuzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Jean-Jacques Ndala kuwa mwamuzi rasmi wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na FAR Rabat.
Ndala ambaye ndiye aliyechezesha fainali ya AFCON 2025 kati ya Senegal na Morocco iliyomalizika kwa goli 1-0 atasaidiwa na waamuzi wenzake kutoka DRC, Guylain Bongele Ngila na Mwanya Gradel Mbilizi, huku Messie Jessie Oved akiteuliwa kuwa mwamuzi wa akiba.
Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Mei 17, 2026 katika Uwanja wa Loftus Versfeld Sundowns watakuwa wenyeji kabla ya marudiano kufanyika wiki moja baadae nchini Morocco.





