pmbet

Mwamuzi wa Senegal na Morrocco afyekwa kombe la dunia

Eric Buyanza

April 10, 2026
Share :

FIFA imemuengua mwamuzi, Jean-Jacques Ndala, kwenye orodha ya wapuliza kipenga wa Kombe la Dunia la 2026.

 

Mwamuzi huyo wa Kongo, aliyechezesha fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Morocco na Senegal, hatakuwepo kwenye mashindano ya msimu huu huko, Marekani, Mexico na Canada.
 

Fainali ya AFCON iligeuka kuwa machafuko na utata, huku Simba wa milima ya Teranga hatimaye wakishinda 1-0 mjini Rabat.

 

Mwamuzi huyo alikosolewa baada ya Senegal kutoka uwanjani kupinga penati waliyopewa Morocco lakini hata waliporudi uwanjani hakuna adhabu aliyoitoa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet