pmbet

Mwana FA aingilia kati ishu ya Rayvanny na Kayumba

Sisti Herman

February 23, 2024
Share :

Baada ya wiki hii kuvuma sana mitandaoni kwa kutoa taarifa kuhusiana na kudai kuwa amedhulumiwa takriban milioni 7 na Rayvanny pamoja na Muongozaji wa video Erick Mzava, mwanamuziki huyo amedai kuwa amepata mualiko kutoka kwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya michezo na burudani Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana Fa kwa ajili ya kupata muafaka wa suala hilo.

 

Kayumba kupitia ukurasa wake wa instagram ame-share picha akiwa pamoja na MwanaFa iliyoambatana na ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa siku ya leo Februari 22 amepokea wito kutoka kwa Waziri MwanaFa kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo walipata wasaa wa kuzungumza ili waweze kupata muafaka wa namna nzuri ya kupata haki yake.

 

Aidha mwisho kabisa Kayumba alitoa shukrani zake kwa Wizara ya Sanaa kwa kum-sapoti, na kumalizia kwa kueleza kuwa mambo yote ameikabidhi Serikali.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet