pmbet

Mwanafunzi afariki kwa kujinyonga kisa kufeli mtihani wa kidato cha nne.

Joyce Shedrack

February 13, 2025
Share :

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limethibitisha kutokea kwa tukio la kifo cha Rabia Paul (19) Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Nyanza Mkazi wa Mtaa wa Barabara ya Msalala Manispaa ya Geita, aliyefariki kwa kujinyonga February 11 Mwaka huu na mwili wake kukutwa ndani ya chumba alichokuwa akiishi ukining'inia kwenye mtandio.

 

Jeshi la Polisi limebaini kuwa tangu januari 26,2025 baada ya matokeo ya mtihani ya Taifa ya kidato cha Nne 2024 kutangazwa na Baraza la Taifa la Mitahani alipatwa gahfla na msongo wa mawazo uliopitiliza ambapo alipata matokeo kinyume cha matarijio yake.

 

Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa jamii kuwa na hofu ya Mungu na kuzifahamu njia za kudhibiti na kukabiliana na msongo wa mawazo ili kuepusha madhara.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet