pmbet

Mwanafunzi wa kidato cha 1 akutwa amefariki akiwa hana mkono.

Joyce Shedrack

October 5, 2026
Share :

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Kizimbani, Raiyan Hemed Amour, amepatikana amefarik Oktoba 4, 2026, baada ya kuanza kutafutwa tangu ijumaa, huku akiwa amekatwa mkono.

Raiyan, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Jimbo la Gando, Zanzibar, amepatikana katika mazingira yaliyomshtua Mbunge wa Jimbo hilo, Salim Mussa Omar, ambaye amelitaka Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo na sababu ya kifo hicho.

Mbunge huyo ametaka hatua kali zichukuliwe iwapo wahusika watabainika, huku akitoa pole kwa familia na wananchi wa Jimbo la Gando, hususan wakazi wa Kwale Mpona.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet