Mwanajeshi aenda jela maisha kwa kuambukiza Ukimwi kwa makusudi
Eric Buyanza
September 27, 2024
Share :

Aliyewahi kuwa mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF), amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumuambikiza mpenzi wake UKIMWI kwa makusudi.
Mahakama ilisema licha ya kufahamu hali yake ya kiafya tangu mwaka 2007, mwanajeshi huyo aliyefahamika kwa jina la Leon Santos Conga bado aliamua kwa makusudi kushiriki ngono isiyo salama na mpenzi wake.





