pmbet

Mwanajeshi mbaroni kwa kujiongeza cheo na kuwa 'Meja'

Eric Buyanza

January 22, 2024
Share :

Baada ya kuona miaka inasonga bila mwajiri wake kumuongeza cheo, mwanajeshi mmoja wa cheo cha chini amefanya kituko cha aina yake baada ya kuamua kujiongezea cheo kivyake.
 

Mwanajeshi huyo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Uganda (UPDF) aliyejulikana kwa jina la Pte Kyambadde alijivika cheo cha 'Meja' na kuanza kutamba mtaani kabla ya kukamatwa.
 

"Jambo la msingi ni kwamba tunaye chini ya ulinzi kwa sababu hiyo. Nimeambiwa amekuwa akijihusisha na uhalifu, lakini bado tunaendelea na uchunguzi," Brig Jenerali Kulayigye alisema.
 

Maelezo yanaonyesha kuwa Pte Kyambandde sio mwanajeshi wa kwanza kujiongeza cheo, kwani visa kama hivyo vimewahi kutokea ambapo mwaka jana mnamo Februari 2023, mwanamke aliyejulikana kama Eunice Keinembabazi alikamatwa kwa kujifanya Kanali wa jeshi. 
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet