pmbet

Mwanamitindo wa Kimataifa akiri kufutwa machozi na Rais Samia.

Joyce Shedrack

December 2, 2024
Share :

Mwanamitindo wa Kimataifa Mellen Happiness Magese, amelezea namna ambavyo Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais alivyoguswa na tatizo lake la maswala ya uzazi na kumsadia.

 

Magese amefunguka hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari huku akikiri wazi kuwa Rais Samia alimfuta machozi na kumwambia mwanangu usilie tena na akaahidi kumuunga mkono kwa kila mali.

 

Mwanamitindo huyo amesema baada ya kutiwa moyo na Rais Samia alipata nguvu ya kupambana upya kuhusu afya yake na kwa sasa Mungu amemjalia mtoto mwenye umri wa miaka 7.

 

Happiness Magese ametangazwa kuwa jaji mkuu wa Tamasha la Samia Fashion Festival litakalofanyika Novemba 30 mwaka huu visiwani Zanzibar.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet