Mwanamke ahukumiwa jela miaka 3 kwa kupatikana na bangi.
Joyce Shedrack
March 13, 2025
Share :
Mahakama ya wilaya ya Ukerewe, mkoa wa Mwanza, imemuhukumu Anastazia Mgaya (41), kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kilogram 5.2.
Mshtakiwa huyo ni mkazi wa kijiji cha mtoni, kata ya Nakatungu, wilaya ya Ukerewe na amepewa adhabu hiyo leo Machi 12,2025 katika kesi namba 5482/2025 iliyokuwa inamkabili.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Lucas Nyehega baada ya kiridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri
Awali akisoma shtaka hilo, mwendesha mashtaka wa Serikali Stephen Kabelela ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 03.03.2025 huko kata ya katunguru, Wilayani humo kinyume na kifungu 17(1)(b) cha Sheria ya dawa za kulevya marejeo ya mwaka 2019.
Hata hivyo mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetetea aliomba mahakama impunguzie adhabu kwakuwa ni mjane na nimbovu wa mguu na amefanya kosa hilo ili aweze kutunza familia jambo lililopingwa vikali na mwendesha mashtaka aliyeomba hakimu atoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.