pmbet

Mwanamke akata uume wa mumewe na kuutupa chooni

Eric Buyanza

December 27, 2023
Share :

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 34 huko jijini Sao Paulo nchini Brazil ametiwa mbaroni baada ya kudaiwa kumkata mumewe uume na 'kuuflashi' chooni.

Mwanamke huyo aliwaambia polisi alifanya hivyo baada ya kugundua mumewe amechepuka na mpwa wake mwenye umri wa miaka 15.

Inaelezwa kwamba siku ya tukio, mwanamke huyo alimshawishi mumewe waende wakalale na alipokubali alimfunga mikono na miguu kitandani, kisha akachomoa wembe na kuukata uume wake.

Katika hali ya kushangaza mwanamke huyo aliupiga kwanza picha uume huo kabla ya kuamua kuutupa chooni.

Baadaye alijisalimisha na kuwaambia Polisi aliamua kuuflashi chooni 'Uume huo' baada ya kuwahi kusikia story kuwa kama ungepatikana ungeweza kuunganishwa na kufanya kazi tena!

Mumewe mwenye umri wa miaka 39, alipatikana akiwa hai na kukimbizwa hospitali lakini hali yake ya kiafya bado haijatengemaa.

Mwanamke huyo yuko kizuizini na anashtakiwa kwa jaribio la mauaji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet