Mwanamke akiri mahakamani kutumia hirizi ili kumtuliza mpenzi
Eric Buyanza
July 25, 2024
Share :
Mwanamke mwenye umri wa miaka 29 kutoka Marapodi huko nchini Zambia amekiri Mahakamani kutumia hirizi itakayomfanya mpenzi wake asiweze kufanya mapenzi na mwanamke mwingine yeyote.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Martha Katongo aliiambia Mahakama kuwa aliamua kufanya hivyo ili kumzuia mwanaume huyo kuzaa hovyo na wanawake tofauti na kisha kutelekeza watoto.