pmbet

Mwanamke apambana na Simba porini ili kumuokoa mumewe

Eric Buyanza

March 9, 2024
Share :

Huko nchini Kenya mwanamke aliyepambana na simba porini akiwa na mumewe ameeleza ni kwa nini alihatarisha maisha yake ili kumuokoa mume wake. 

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Susan, anasema hakuweza kutazama tu simba akijaribu kumuua mumewe ingawa awali alikimbia. 

Mama huyo wa mtoto mmoja anasema ni "mapenzi tu aliyonayo kwa mumewe" ndiyo yaliyompa ujasiri wa kurudi kupambana na mnyama huyo hatari. 

"Hatukua tunatarajia, mzee alikua mbele mimi nyuma, simba alikua ndani ya miti nilipomuona mimi nikakimbia nikampita. Simba akaenda ghafla akamrukia mume wangu" anasimulia Susan. 

Mume wake (Michael) alijaribu kupambana na simba huyo huku akiwa amemkaba shingo lakini baada ya kung'twa kwenye mguu na mkono aliishiwa nguvu na kuomba msaada kwa mkewe. 

Susan hakusita alimrukia simba huyo na kumkata kwa panga, kitendo kilichoweza kumuinua mume wake na kumalizia kazi ya kumuua simba huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet