Mwanamke mporaji wa mabenki kwa silaha atupwa jela miaka 30
Eric Buyanza
May 28, 2026
Share :

Aliyekuwa mfuasi wa kundi la Red Army Faction (RAF) la Ujerumani amehukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani kwa kutekeleza vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha kati ya mwaka 1999 na 2016.
Daniela Klette, mwenye umri wa miaka 67, alikamatwa katika nyumba moja mjini Berlin mwaka 2024 baada ya zaidi ya miaka 30 akiwa mafichoni.Kesi yake ilianza kusikilizwa mwaka uliopita.
Wakili wake wa utetezi aliomba aachiliwe huru, lakini mahakama ya Verden, Lower Saxony, ilimkuta na hatia siku ya Jumatano kwa makosa ya ujambazi uliokithiri na makosa mengine ya kihalifu.
Kundi la RAF lililojulikana pia kwa jila la “Baader-Meinhof Gang,” lilifahamika zaidi kwa kufanya mauaji, utekaji nyara na mashambulizi ya mabomu kuanzia miaka ya 1970 hadi mapema miaka ya 1990.
Mahakama ilielezwa kuwa Daniela Klette alihusika katika uporaji wa maduka makubwa na magari ya kubeba fedha akishirikiana na wenzake wawili Burkhard Garweg na Ernst-Volker Staub, ambao bado hawajakamatwa.





