Mwanamke mzee zaidi duniani afariki akiwa na umri wa miaka 122
Eric Buyanza
February 4, 2025
Share :
Lin Shemu, anayeaminika kuwa mwanamke mzee zaidi duniani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 122 baada ya kuaga dunia kwa amani akiwa amelala nyumbani kwake katika jimbo la Fujian nchini China.
Lin Shemu, alizaliwa Juni 18, 1902, alishuhudia vita viwili vya dunia na aliishi maisha yake yote katika jimbo la Fujian, lililoko kati ya Shanghai na Hong Kong.
Lin na marehemu mume wake walijaaliwa watoto watatu wa kiume na wanne wa kike,
mtoto wake mdogo kwasasa ana umri wa miaka 77.
Mbali na kupoteza uwezo wa kuona kutokana na uzee na kuumia miguu yote miwili baada ya kuanguka, Lin hakuugua magonjwa mengine yoyote na aliweza kujihudumia maisha yake yote.
Bibi huyu alikuwa na umri wa miaka 10 wakati meli ya Titanic ilipozama mwaka wa 1912.