Mwanamke wa kichina matatani baada ya kujifungua mtoto mweusi
Eric Buyanza
December 11, 2024
Share :
Mwanamke mmoja wa kichina aliyeianza siku yake kwa furaha baada ya kujifungua mtoto mwenye afya njema, ghafla siku hiyo iligeuka na kuwa kama ndoto ya kutisha baada ya mume wake kutaka kufanyike vipimo vya nasaba (DNA) kwakuwa mke wake alikuwa amejifungua mtoto mweusi.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka jiji la Shanghai anasimulia kisa hicho akisema baada ya kujifungua na ilipofika muda wa mumewe kumuona mtoto, mume huyo alikaa mbali akimuangalia kwa mshangao na kukataa kumbeba.
Katika hali ya kushangaza mwanamke huyo nae akasema alishangazwa na rangi ya mtoto wake alipomuona kwa mara ya kwanza huku nae akisisitiza anataka ufafanuzi kutoka kwa madaktari kwani hajawahi kufika Afrika na wala hamjui mtu mweusi yoyote.
“Jambo hili laweza kutokea kiasili kwa watoto wachanga kwa sababu tishu zao za ngozi ni nyembamba na mzunguko wao wa damu sio mzuri,”
"Ni kawaida kwasababu baada ya muda rangi hubadilika na kuwa nyeupe." mtaalamu mmoja wa afya alisema.
Mwanamke huyo hatimae alikubali kufanyiwa vipimo lakini wengi walirusha lawama kwa mume wake kwa kuonesha kukosa imani na mke wake.