Mwanamke wa kizungu aliyejipiga sindano za kuwa mweusi
Eric Buyanza
March 19, 2025
Share :
Martina Big anayetokea nchini Ujerumani na mumewe Michael Eurwen, wote wawili wamejidunga sindano ya homoni ya Melanotan ambayo huchochea seli na kufanya ngozi zao kuwa nyeusi.
Martina ambaye pia ana matiti makubwa aliyoyapata baada ya kufanyiwa upasuaji amedai amepokea mialiko mingi kutoka kwa mashabiki zake katika nchi nyingi za Afrika, jambo linalowafanya yeye na mpenzi wake kufikiria kuhamia afrika.
"Mimi na mume wangu tayari tulikuwa tumepanga kuhama miaka michache iliyopita, tumepokea mialiko kutoka kwa mashabiki katika nchi nyingi za Afrika na kwa hivyo haikuwa rahisi kuchagua. Kwa sasa, tuna Kenya na Namibia kwenye orodha yetu fupi.
"Kwa kuwa kazi zangu nyingi za uanamitindo ziko Ulaya na Marekani, Michael anahofia itakuwa vigumu kwangu kupata pesa barani Afrika. Imebidi kufanya kazi ya ziada kumshawishi kwamba huu ni uamuzi bora kwetu."
Pamoja na uboreshaji wa matiti, Martina ameongeza ukubwa wa 'Lips' zake na ana mpango wa kuongeza makalio kabla ya kuelekea Afrika.
Alisema: "Mimi na mume wangu bado tunafanyia kazi ratiba. Ni muhimu sana nifanye upasuaji wa kuongeza makalio na pua hapa Ulaya kabla ya kuelekea Afrika.
"Nataka kuhamia Afrika kwa sababu ninahisi nina uhusiano wa kina na watu wa Afrika.” alisema Martina.