Mwanariadha achomwa moto wa petroli na mpenzi wake wa zamani.
Joyce Shedrack
September 3, 2024
Share :
Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei amenusurika kifo baada ya kuchomwa moto wa petroli na mpenzi wake Dickson Ndiema nyumbani kwake Nchini Kenya ambako alikuwa akifanaya mazoezi.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya hivi karibuni mjini Paris na kushika nafasi ya 44 ameungua kwa zaidi ya asilimia 75 ya mwili wake na amelazwa akiwa mahututi katika hospitali moja nchini Kenya.
Jeshi la Polisi Nchini Kenya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Jumapili katika mji wa Endebess Magharibi ya Kenya na kueleza kuwa mwanaume huyo ambaye alikuwa na petroli alimwangia mpenzi wake kabla ya kumteketeza.
Aidha, polisi wanasema mwanaume huyo naye pia alijeruhiwa kutokana na miale ya moto na wote wamelazwa katika hospitali ya moyo Nchini Kenya.