pmbet

Mwanariadha anayeshilikia rekodi ya dunia afariki Kenya

Sisti Herman

February 12, 2024
Share :

Mwanariadha wa mbio ndefu kutoka nchini Kenya, Kelvin Kiptum ambaye anashikilia rekodi ya dunia kukimbia kwa muda mfupi zaidi na ‘kocha’ wake raia wa Rwanda, Garvais Hakizimana wamefariki dunia kwa ajali ya gari, jana Jumapili katika eneo la Kaptagat nchini humo.

Inaelezwa gari hiyo aina ya Toyota iliyokuwa ikiendeshwa na Kiptum ilikuwa na jumla ya watu watatu akiwemo mwanamke mmoja, ilipoteza muelekeo na kwenda kugonga mti mkubwa.

Hata hivyo katika ajali hiyo Kiptum na kocha wake walifariki dunia huku mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Sharon Kosgey akikimbizwa hospitali kutokana na majeraha aliyopata.

 

Kiptum kwa mujibu wa mtandao wa World Athlethic record ndiye anayeshikilia rekodi ya kukimbia Marathon kwa masaa 2:00:35 aliyoiweka mwezi Oktoba mwaka jana.

Kiptum amefariki akiwa na umri wa miaka 24 aliwahi kushinda tuzo tatu ikiwemo ‘World Marathon Majors’ (WMM), zilizofanyika Desemba 2022 na Oktoba 2023.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet