Mwanasheria wa Chasambi; Simba wamwamini Mgunda amerudisha Umoja
Sisti Herman
May 17, 2024
Share :
Mwanasheria wa michezo Happyness Basil Florence ambaye anamsimamia kiungo wa klabu ya Simba na mchezaji bora wa michuano ya vijana chini ya miaka 20 kwa miaka miwili mfululizo Ladack Chasambi kupitia kampuni ya Football Fratenity amesema klabu hiyo inapaswa kumwamini kaimu kocha Mkuu wa klabu hiyo Juma Mgunda kutokana na mabadiliko chanya aliyoyaongeza kwenye timu hiyo katika kipindi kifupi.
Anaandika Happyness kupitia ukurasa wake wa Instagram wa @micc_lawyer
"Ndiyo ni Juma Mgunda na Simba, ni yapi nimejifunza,
mimi si mchambuzi wa mpira ,ila mtazamaji na mwenye kupenda kufikiri.
"Mgunda ni kocha ambaye haaminiki tu kwa sababu yeye ni mzawa ,waswahili wanasema Nabii hakubaliki kwao .
"Ndiyo, Mtu huyu kwa muda mchache amerudisha kitu kikubwa kilichokua kinakosekana kwa wachezaji , na hiki kinaisumbua sana Simba , na ndicho upande wa pili wamefanikiwa sana. Mwalimu wa saikolojia wa Simba naweza sema hakutosha kwenye upande wa wachezaji kuwa na umoja na hiki nilikua nakiona kupitia namna ambayo wachezaji wana 'behave' uwanjani , yaani hata likifungwa goli huoni mzuka wa kushangilia.
"Hii ni mbaya sana… mtu anaweza sema sio lazima, au ni kawaida timu fulani…… lakini jiulize (high achievement) timu au mchezaji nini ? kama sio kufunga goli ama kipa kudaka penalty?
"Ni sawa na maisha ya kawiada uwe unapambania dili yako fulani alafu itiki alafu usiwe kwenye kilele cha furaha , basi ujue kunashida mahali kwa maana kwa hali ya kawaida lazima ufurahi. Mtazame david kameta, ile hali inapaswa kuonekana sana kwa kila mchezaji na hii huwa inawapa sana hali ya ushindani na mara nyingi ushindi.
"Funzo la pili, kila mtu anauwezo wa kufanya jambo akiaminiwa ,watazame vijana ambao hawakuaminika , walikua chaguo la pili, umuhimu wa 'rotation' unaoneka 'passion', na uhitaji wa upambanaji wa hali ya juu ndani yao iko wazi.
"Hata kwenye maisha ya kawaida Usidharau raslimali ulizonazo zitumie wakati ukitafuta kubwa zaidi.
Tusikate tamaa , kwa hali yeyote ile , unaemuona hakufai ndio atakuokoa nyakati usizozitarajia. mipango ya Mungu mwanadamu ,ataichelewesha tu lakini hataizuia.
"Subira na Mungu ndio Gate Pass"..
Alimaliza kuandika Mwanasheria huyo.
Yapi maoni yako?