Mwanasheria wa Yanga akiri klabu hiyo kushtakiwa na baadhi ya wazee wa timu.
Joyce Shedrack
July 17, 2024
Share :
Mkurugenzi wa Washeria wa Klabu ya Yanga amezungumza haya kufuatia taarifa za baaadhi ya wazee wa klabu hiyo kutaka uongozi wa yanga chini ya Eng. Hersi uachie ngazi.
“Mei 2024 walalamikaji walipeleka maombi ya kukazia hukumu kwa Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba Mahakama kulifuta baraza la wadhamini wa Yanga na kuutoa uongozi wa Yanga na kutaka wakabidhiwe timu na Asset zote za Yanga waendeshe wao.
“Baada ya kufanya hivyo Juni 10, 2024 klabu ilipata taarifa kwamba kuna kundi la watu wamepeleka maombi Mahakami kuomba uongozi wa Yanga uondolewe na wakabidhiwe klabu hiyo.
“Uongozi wa Yanga chini ya Rais Eng. Hersi na Jopo la mawakili tulianza kufuatilia suala hilo na kugundua kuwa, kesi hiyo iliendeshwa kwa upande mmoja kwa hawa watu kugawana majukumu kwa upande wa mlalamikaji na mlalamikiwa.
“Tuligundua Juma Ally Abeid aligushi sahihi ya Klabu na kujifanya mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa klabu, aligushi sahihi ya Mama Fatma Karume akijidai mwakilishi wake, aligushi sahihi la Mzee wetu Jabil Katundu ambaye alilazimishwa kuingia kwenye hili shauri,” Simon Patrick, Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC.