Mwanaume afunga ndoa Hospitalini akiwa amelazwa
Eric Buyanza
December 12, 2023
Share :
Mwanaume mmoja huko Afrika Kusini amefunga ndoa akiwa kwenye kitanda cha Hospitali baada siku ya ndoa yake kumkuta akiwa wodini anaumwa.
Tukio hilo lililowashangaza wengi limetokea kwenye Hospitali ya Far East Rand, huku likishudiwa na ndugu pamoja na familia.
Inaelezwa kuwa Hospitali hiyo ilitoa ruhusa ya kufungwa kwa ndoa hiyo huku ikishiriki kwa asilimia kubwa katika maandalizi ndani ya wodi hiyo.