Mwanaume wa miaka 48, anayetanua na mpenzi wa miaka 103
Eric Buyanza
February 2, 2024
Share :
Wakili mwenye umri wa miaka 48 anadai kuwa anampenda kupita maelezo mpenzi wake mwenye umri wa miaka 103, licha ya maneno mengi yanayosemwa kila kona juu yao.
Mart Soeson, kutoka Estonia, amekuwa kwenye uhusiano na Bibi huyo aitwae Elfriede Riit tangu mwaka 2013.
Bi Riit ambaye pia ni mzaliwa Estonia, atasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya mwaka wa 104 baadaye mwezi huu wa Februari.
Wapenzi hao wanasisitiza kuwa kupishana kwao umri kwa miaka 55 hakumaanishi chochote kwao na ni bora watu wakawaacha waendelee kuenjoy na mapenzi yao badala ya kuendelea kuwasema kila kukicha.