Mwandamizi Charles Abel amjibu vikali kwa hoja Mamadou Gaye kuhusu AFCON 2027
Sisti Herman
January 18, 2026
Share :

Kufuatia Chapisho lililopita la ukurasa huu kuhusu Mwanahabari wa Ivory Coast, Mamadou Gaye kufanya mashambulizi makali dhidi ya nchi tatu za Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda) zinazotarajiwa kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya afrika AFCON 2027, akiweka shaka juu ya uwezo wao wa kufikia viwango vya michuano hiyo, Mwandishi wa habari Mwandamizi na Mchambuzi wa Mwanachi Communication Limited Charles Abel amejibu vikali mashambulizi ya Gaye kwa hoja.
Kupitia moja ya majukwaa ya michezo, @charlesabel24 ameandika hivi;
_______________
Niliwahi kuambiwa na mwalimu wangu mmoja hivi kuwa unaweza kupata picha ya maudhui ya kitabu kabla hujakisoma kwa kuangalia historia ya mwandishi.
Mfano, Hayati Mwalimu Nyerere hakuupenda na alikuwa adui mkubwa wa Ubepari. Usitegemee angeandika kitabu na kuusifu Ubepari.
Mfano huu nautumia kwa Mamadou Gaye. Katika CHAN alikasirika kisa nchi za Afrika Mashariki ziligoma kutoa free visaz na aliwahi kusema hadharani kuwa amezipa kadi nyekundu Tanzania na Uganda.
Mtu kama huyo tayari ana kasumba mbaya na East Africa kwa sababu ya maslahi yake.
Lakini swali lake ama ni la kipuuzi au kaweka mfano kichuki.
Utafiti wa Business Insider Africa umeziweka Kenya na Tanzania katika orodha ya nchi 10 zenye miundombinu bora zaidi ya Barabara barani Afrika. Yeye swali lake limebase katika uthibitisho upi?
Uthibitisho ni huu
https://africa.businessinsider.com/local/lifestyle/10-african-countries-with-the-best-road-quality-infrastructure/fqd5sl8
_______________
Awali Mamadou Gaye alinukuuliwa akisema hivi wakati wa mkutano wa Rais wa CAF Patrice Motsepe na waandishi.
“Inayofuata (AFCON) inaelekea nchi 3 za Afrika Mashariki ambako tayari nimefika, hakuna barabara ndani ya nchi, baadhi ya wenzangu kutoka Afrika Mashariki waliniambia kutoka nchi moja hadi nyingine itakuchukua siku 2 kuendesha gari"
"Halafu wasiwasi wangu mkubwa, na wengi wana wasiwasi, je tutashusha viwango kwa kwenda Afrika Mashariki, suluhu ni nini mbele?"
Hizi zilikuwa sehemu ya nukuu zake wakati wa mkutano wa Rais wa CAF Patrice Motsepe na waandishi.





